TANROADS TABORA YAREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA YA BUKUMBI - KAHAMA


Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora imefanikiwa kurejesha mawasiliano ya barabara ya Bukumbi kuelekea Kahama ambayo ilikatika kutokana na gari la mizigo kuzidisha uzito kisha kupasua Kalvati ambalo lilisababisha maji ya mvua kusambaa kwenye eneo lenye urefu wa Kilomita 1.2 kati ya hizo mita 800 zipo upande wa Tabora na mita 400 upande wa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa wa Mkoa tarehe 17 Disemba 2023; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Mhandisi Raphael  Mlimaji amesema eneo la barabara lililokatika ni Kati ya Kijiji cha Muhulidede Kata ya Ishihimulwa, Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora Kilomita 108 kufika Tabora mjini na Kijiji cha Busule kata ya chona, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga; kutoka eneo la tukio mpaka Kahama kuna umbali wa Kilomita 4.

Amesema mnano tarehe 14 Disemba 2023, majira ya saa tisa usiku gari la mizigo aina ya fuso lililokuwa limebeba shehena ya Karanga lilipita katika barabara hiyo inayounganisha Mkoa wa Tabora na Shinyanga kupitia Wilaya za Uyui na Kahama, kutokana na kuzidisha uzito na siku hiyo mvua kubwa zilinyesha eneo hilo gari hiyo ilipasua Kalvati ambazo zilijengwa zamani kwenye barabara hiyo ambayo awali ilikuwa ni ya Halmashauri na baadae kuletwa TANROADS ili ifunguliwe iwe inapitika na Wananchi.

Amesema kufuatia athari hiyo TANROADS imeamua kukata maeneo manne tofauti na kupanga mawe ili kuwezesha maji yatakayokuwa yameongezeka kupita chini wakati vyombo vya moto na watu wakipita juu ya barabara pasipo kusimama kwa huduma za usafiri na usafirishaji kwani barabara hiyo inapitisha shehena nyingi zinazotoka Mikoa mbambali ikiwemo Katavi, Mbeya na maeneo ya Jirani kutokana na uwepo wa Maghala mengi ya chakula Kahama ambayo yanahudumia Nchi za Burundi, Rwanda na Kenya.

Mha. Raphael Mlimaji ameeleza kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa sasa Barabara hiyo inapitika kwa asilimia 100 na kwamba kutokana na ufupi wa barabara hiyo magari mengi yamekuwa yakipita katika barabara hiyo hasa nyakati za usiku kwa sababu wanaona wakipita mchana wanaweza wakashtukizwa kwa kuwekewa Mzani wa mkeka kwa jili ya kupima uzito kwa hiyo nitoe wito kwa wenye vyombo vya moto kuacha kuzidisha mizigo kwani wanaharibu miundombinu na  ni kinyume na sheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post