TET YASAINI HATI YA MAKUBALIANO NA TAASISI BINAFSI KUBORESHA ELIMU NCHINI


Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mapema tarehe 29/11/2023 imesaini makubaliano na taasisi tano zisizo za kiserikali yenye  lengo la kuboresha elimu nchini katika nyanja mbalimbali.

Taasisi  hizo ni pamoja na Project Zawadi ambao wameingia makubaliano ya kutoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi kwa kutoa  nyezo  bora za mafunzo, Taasisi ya  OCODE yenyewe itahusika na kuwafundisha wanafunzi na walimu stadi za maisha ambazo zitaweza kuwasaidia katika maisha ya kila siku.

Taasisi nyingine ni Jenga Hub yenyewe imeingia makubaliano ya kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya teknolojia kwa walimu na wanafunzi, Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope itatoa mafunzo ya lugha ya alama kuanzia ngazi ya Awali hadi vyuo vya ualimu.

Taasisi nyingine ni Right To Play ambayo itaweka maudhui ya miongozo mbalimbali ya mbinu za kusoma kwa njia ya michezo kidigitali (digitization of teaching and learning materials).

Akizungumza mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema kuwa, Taasisi ya Elimu Tanzania inathamini mchango wa wadau unaoendelea kutolewa katika kuboresha elimu nchini huku akisisitiza TET itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali katika eneo la elimu.

“Ninashukuru sana namna ambavyo mmeamua kushirikiana pamoja na sisi, ni suala ambalo Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya  wa Tanzania analisisitiza katika kuweka ushirikiano na wadau mbalimbali katika kutekeleza majukumu ya Serikali kwa  namna ya kuhakikisha wanafunzi nchini wanapata elimu iliyo bora”. Amesema Dkt. Komba.

Ameongeza kwa kusema kuwa makubaliano haya yamekuja wakati muafaka ambapo kumefanyika maboresho ya Sera na Mitaala ya Elimu nchini  ambapo kupitia wadau waliongia makubaliano katika  kuhakikisha maboresho yaliyofanyika yanatekelezwa.

Kwa upande wa Taasisi hizo zilizoingia makubaliano na TET zimeishukuru Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya ushirikiano unaotoa nafasi kwa Taasisi zisizo za Serikali kufanya kazi kwa ubora katika kuwahudumia wananchi hasa katika eneo la Elimu.

Taasisi hizo ni pamoja na Organization for Community Development iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Bw.  Joseph Jackson, Fondation for Disabailities Hope iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Maiko Salali, Right To Play iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkazi, Bi.Maria Mongi, Taasisi ya Jenga Hub iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Bi Nancy Sumary, Project Zawadi iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Brian Singer.

Post a Comment

Previous Post Next Post