MAHAWANGA AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE KATA YA NDUGUMBI NA KUSISITIZA USHIRIKIANO


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Mahawanga  Janeth  amezinduzi  Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika Kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa kufanya ziara ya kukutana na Wanawake  sambamba  na Vijana na Mabinti ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. 

Uzinduzi  huo umeweza kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali  kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni  sambamba na Viongozi wa Chama na Jumuiya zake vilevile Viongozi  wa Umoja wa Wanawake  kutoka Kata jirani sambamba na Wanachama wa Majukwaa kutoka Vikundi 197 vya Kata ya Ndugumbi.

Mhe. Mahawanga  kupitia Uzinduzi huo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  ambaye ndiyo Muasisi wa Majukwaa kwa maono chanya na kiu yake ya kuwakwamua Wanawake  kiuchumi kupitia fursa mbalimbali.

Mh. Mahawanga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kwa kuwawezesha Wanawake wa Kata ya Ndugumbi kwa kupitia mikopo ya 10% kwa kuwawezesha kiasi cha 380,716,000/= kwa mwaka 2021 - 2023 sambamba na Wanawake 151 kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo ya haki za Wanawake, Biashara, Ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali. Elimu ya afya ya uzazi, Fursa n.k

Aidha Mhe. Mahawanga amesisitiza ili majukwaa  yaweze kuendelea na kuwa imara ni muhimu Viongozi na wanachama kuendeleza  upendo, ushirikiano, kuchangamkia fursa zinazotuzunguka, kuwa wabunifu sambamba na kumtanguliza Mungu katika shughuli za kila siku.

Mhe. Mahawanga  amekemea vikali vitendo vya kutokuheshimiana katika jukwaa na kuwataka wanachama na Viongozi  kuheshimiana, kukosoana kwa staha, kusameheana wanapotofautiana na kusimamia malengo mahususi ya majukwaa kama inavyoelekeza miongozo ya majukwaa.

Aidha Mhe. Mahawanga  amewaahidi kuwa nao bega kwa bega kuhakikisha Jukwaa la Wanawake Kata ya Ndugumbi  pamoja na Majukwaa yote ya Mkoa wa Dar es Salaam yanafanikiwa pamoja na kuendelea kupokea changamoto  zote na kuzifanyia kazi.

Pia Mhe. Mahawanga amewasisitiza Wanamajukwaa kuelekea  Ucahguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Wanawake wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu na kugombea nafasi za Uongozi.

Post a Comment

Previous Post Next Post