Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuzindua ripoti ya tafiti ya afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2022.
Tafiti hii hufanyika nchini kila baada ya miaka 5 kupitia Ofisi za Mtakwimu Mkuu wa Tanzania Bara na Zanzibari kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pande zote mbili na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau ambapo Ripoti hutoa dira juu ya hali halisi ya utolewaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto.
Tafiti hii huongoza kwenye tathmini ya uwajibikaji katika kutatua changamoto za utoaji wa huduma za afya uzazi kwa kupima viashiria vilivyopo na jinsi tulivyofikia malengo ya utoaji wa huduma bora za afya ya uzazi pamoja na kupunguza au kuondokana na athari zitokanazo na changamoto za afya ya uzazi
Sambamba na uzinduzi wa Ripoti hii Rais Dkt. Samia anatarajiwa pia kuzindua magari ya kubebea wagonjwa, magari ya usimamizi pamoja na kugawa vifaa tiba nchi nzima ikiwa ni muendelezo wa azma yake ya kuboresha huduma za afya nchini.