DKT. MPANGO ASISITIZA ULINZI WA MAZINGIRA, PAMOJA NA VYANZO VYA MAJI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango amekemea tabia ya uharibifu wa mazingira na matumizi mabaya ya vyanzo vya maji, na kutaka kila mwananchi awe mlinzi wa mazingira.

Kufuatia hilo, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameitaka jamii kushiriki kubeba jukumu la kulinda na kutunza rasilimali za maji kwa faida ya matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha Nishati ya umeme, Kilimo na matumizi mengine ya muhimu kwa kijamii,na kwamba kwa vyanzo vya maji vilivyoharibiwa na kukauka iwe fundisho kwa wengine kutoharibu rasilimali za maji.



Ametoa tahadhari hiyo ili jamii iendelee kulinda, kutunza na kuendeleza rasilimali za maji zilizopo katika kila kona ya nchi kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Akitoa salamu na shukrani, Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.7, na hivi sasa wilaya ya Makete imekuwa ya kwanza kitaifa kwenye upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 99.

Makamu wa Rais yupo mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 26 Oktoba, 2023, ambapo Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) anashiriki ziara hiyo.




Post a Comment

Previous Post Next Post