RAIS SAMIA AWANUSURU WANACHI ITELEFYA KUEPUKANA NA KULIWA NA MAMBA WAKIFUATA MAJI



Waziri wa maji wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameweka jiwe la msingi katika  mradi wa maji katika kijiji cha Itelefya uliogharimu kiasi cha 348,757,051.47 wilaya Momba ambao utazinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwezi ujao mwaka huu.

Mradi huu tayari unatoa huduma kwa wananchi na unanufaisha wananchi zaidi ya 2,448.


Akizingumza mbele ya Waziri wa Maji Diwani wa Itelefya Wilaya ya Momba ameeleza kuwa mradi huu umewanusuru wakina mama wa Itelefya waliokua wakitembea umbali mrefu kutafuta maji na wakati mwingine kukumba na  vifo kutokana na kuliwa na mamba.


Wananchi wa kijiji cha Itelefya wameupokea mrad huu wa maji kwa shangwe na wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mradi huu kutekelezwa hasa kutokana na wananchi wa kijiji cha Itelefya adha waliyokuwa wakiipata ikiwa ni pamoja na kuliwa na mamba wakati wakihangaika kutafuta huduma ya maji.

Post a Comment

Previous Post Next Post