PROF.MKUMBO AFANYA ZIARA YA SIKU MOJA ZANZIBAR



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amefanya ziara ya siku moja Zanzibar tarehe 5 Agosti, 2023, ikiwa na lengo la kukutana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ili kujitambulisha na kufanya mazungumzo, hii ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri na kuunda Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na kisha kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa waziri wake na Dkt. Tausi Kida kuwa Katibu Mkuu. 


Pamoja na kukutana na Rais Mwinyi, Prof. Mkumbo pia alikutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar Mhe. Mudrik Soraga, ambapo katika mazungumzo yao, kwa pamoja walisisiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kwatika kukuza uwekezaji ili kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla. 


Aidha, Pro. Mkumbo pamoja na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea eneo la uwekezaji wa bandari kubwa inayojengwa Zanzibar eneo la Mangapwani. 


Ujumbe ulioongozana na Waziri Prof.Kitila ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji  Dk.Tausi Kida, Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu EPZA Bw. Charles Itembe, Mkurugenzi Mkuu TIC  Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi wa Miundombinu wa Mamlaka ya Bandari Dkt.Hussein Lufunyo Wakurugenzi wa Wizara.

Post a Comment

Previous Post Next Post