AWESO AELEKEZA MILION 500 NA MIEZI MITATU MAJI YAPATIKANE



Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuanza mipango ya kuongeza Bajeti ya Maji kwa wilaya ya Momba baada ya kufanya ziara kwa kina sana na kufanya tathmini ya uhitaji wa jimbo hili ambalo jografia yake ni ya aina yake.


Katika hatua nyingine, Diwani wa Kata ya Kamsamba Wilayani Momba, Kyalambwene Joshua Kakwale amejilaza chini kama ishara ya msisitizo kumuomba Waziri wa Maji Jumaa Aweso afanikishe Kata hiyo kupata maji kwani Wakazi wake wanateseka ikiwemo baadhi ya Watu kuliwa na mamba wakati wakichota maji mtoni.


Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye alikuwa kwenye ziara ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maji katika mkoa wa Songwe wilaya ya Momba amekiri Momba ina changamoto na kazi kubwa inatakiwa kufanyika.

Akijibu ombi la Diwani, ameahidi kuwa Serikali itapeleka TSh500 milioni ndani ya wiki mbili kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji utakao kuwa Suluhu ya changamoto ya Maji katika eneo hilo lenye wakazi wengi.

Waziri Aweso amewaahidi ndani ya miezi mitatu mradi utakamilika na huduma itapatikana.

Post a Comment

Previous Post Next Post