Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazidi kuunga mkono mipango ya kitaifa inayohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), mifumo wezeshi ya kidijjiti pamoja na Masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STUH/STEM).
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema hayo wakati akifungua mkutano wa Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) na waandishi wa Habari, kuhusu mafanikio ya Tanzania kwenye mashindano ya Hisabati, Afrika na ulimwenguni. Mkutano huo umefanyika katika ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam, 24 Septemba 2026.
Mhandisi Peter ametoa pongezi kwa CHAHITA, kwa kuratibu ushiriki wa nchi kwenye mashindano hayo, na kupelekea Tanzania kuwa na matokeo bora kila mwaka hadi kufikia kuwa nafasi ya 5 bora kati ya nchi 26, na kwa mara ya kwanza kupata medali ya dhahabu ya mshindi wa kwanza kwa wasichana kutoka Afrika katika mashindano ya Dunia ya Hisabati (International Mathematical Olympiad – IMO 2026) yaliyofanyika Shanghai, China.
TCRA imeendelea kufadhili ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya hisabati ya shule za sekondari Afrika na Kimataifa yaani mashindano ya Olimpiki ya Hisabati ya Afrika (PAMO) na Olimpiki ya Kimataifa ya Hisabati (IMO) tangu mwaka 2023 ambapo Tanzania ilianza rasmi kushiriki mashindano hayo.
Mwasalyanda, ameelezea kuwa TCRA imejizatiti kuwajengea uwezo vijana ili washiriki kikamilifu katika kuijenga Tanzania ya kidijitali kupita ubunifu na matumizi ya mifumo wezeshi ya TEHAMA. Hadi sasa TCRA imehamashisha uanzishwaji wa vilabu 800 vya kidijiti, kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu nchini, kwa lengo la kuchagiza upatikanaji wa wabunifu wenye uwezo wa kutengeneza suluhu za kidijiti kwa changamoto za jamii.
#tcratz #PAMO #IMO #STEM #Tanzania
