MWENYEKITI MSAKUZI KUSINI AWASHUKURU MHE. KAIRUKI NA MHE. NYANTORI KWA UJENZI WA SEKONDARI


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msakuzi Kusini kata ya mbezi, Mhe. Luena, ametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mheshimiwa Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, pamoja na Diwani wa Kata ya Mkezi, Mheshimiwa Pius Nyantori, kwa mchango wao katika kuleta fedha za ujenzi wa Sekondari ya Ghorofa katika eneo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mtaa wa Msakuzi Kusini, Mwenyekiti Luena amesema wananchi wamekuwa na kiu ya muda mrefu ya kupata shule ya sekondari, na kwamba hatua ya kupatikana kwa fedha za ujenzi imeleta matumaini mapya kwa wananchi.

“Kwa niaba ya wananchi wangu wa Mtaa wa Msakuzi Kusini, napenda kutoa shukrani kubwa sana kwa Mbunge wetu mpendwa Mhe. Angellah Kairuki na Diwani wetu mpendwa Mhe. Pius Nyantori kwa kutuletea fedha za ujenzi wa Sekondari ya Gorofa. Kwa miaka mingi wananchi walikuwa na kiu ya kupata maendeleo na kujengewa sekondari, lakini uongozi wenu umefanikisha jambo hili,” amesema Luena.

Mwenyekiti huyo amewashukuru viongozi hao kwa hatua hiyo na kuwaomba waendelee kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele maendeleo ya eneo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post