TCRA NA RURA ZABADILISHANA UZOEFU KATIKA USIMAMIZI SEKTA YA MAWASILIANO


Ujumbe wa watu wanne (4) kutoka Rwanda Utilities Regulatory Authority (RURA) @rwanda_utilities_regulator umefanya ziara ya kimafunzo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora katika udhibiti na uendelezaji wa sekta ya mawasiliano.

Ujumbe huo uliongozwa na Bw. Charles GAHUNGU, Mkuu wa Sekta ya TEHAMA (General Manager of ICT Regulation), ambaye aliambatana na Bw. Jean d’Amour TUYIZERE, Bw. KARASIRA Denis na Bw. Jean Pierre BIZIMANA wataalamu kutoka idara hiyo.

Ujumbe wa RURA ulipata fursa ya kujifunza kuhusu namna TCRA inavyotekeleza majukumu yake ya udhibiti wa sekta ya mawasiliano, ikiwemo mifumo,taratibu na uzoefu mbalimbali unaotumika katika kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, ziara hiyo imekuwa fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto, mafanikio, ubunifu na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na taasisi hizo katika kutekeleza majukumu yake ya udhibiti.

Huu ni mwendelezo wa ziara mbalimbali za mafunzo, ambazo zimekuwa zikifanyika na mamlaka za mawasiliano mbalimbali kuja TCRA, kubadilishana uzoefu wa jinsi bora ya kusimamia Sekta ya Mawasiliano. Mpaka sasa tumepokea ujumbe kutoka Mamlaka za Usimamizi wa Mawasiliano kutoka nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Msumbiji, Mali, Comoro, Zambia, Afrika Kusini na Zimbabwe walitembelea TCRA.


#tcratz #rura #regulators #tanzania

Post a Comment

Previous Post Next Post