TUZO KWA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN


Tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua uongozi wake na dhamira yake ya kuhakikisha Mradi wa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) unakamilishwa kwa mafanikio.

Alipoingia madarakani, ujenzi wa mradi ulikuwa umefikia takribani asilimia 30. Chini ya uongozi wake, Serikali iliendelea na utekelezaji wa mradi huo kwa kutumia mapato ya ndani, hadi kukamilika kwa mafanikio.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa pamoja na Mawaziri wastaafu wa Wizara ya Nishati- Mhe. Dkt. Medard Kalemani, Prof. Sospeter Muhongo, Mhe. January Makamba na Mhe. Dkt. Dotto Biteko- pamoja na Waziri wa Nishati wa sasa, Mhe. Deogratius Ndejembi, na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu.

Uongozi wenye maono, dhamira na uzalendo umewezesha ndoto ya Taifa kuwa kweli.

Post a Comment

Previous Post Next Post