TARURA, UDSM-COET KUJADILI USHIRIKIANO KATIKA UTAFITI NA MASUALA YA KIHANDISI


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekutana na Ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sehemu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET)  na kufanya kikao cha kubadilishana uzoefu katika nyanja ya Kihandisi. 

Kaimu Mtendaji Mkuu wa (TARURA) Mhandisi Edward Amboka  ameueleza ujumbe huo kuwa kuna umuhimu wa taasisi hizo kushirikiana  katika maeneo ya utafiti  na kwamba TARURA ipo tayari kushirikiana nao.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo, Sehemu ya Uhandisi na Teknolojia (COET) Dkt. Macha amesema Chuo cha Uhandisi na Teknolojia kimefanya maboresho mbalimbali kwenye maeneo ya utafiti na ufundishaji na kwa sasa wameona ipo haja ya kufanya kazi kwa pamoja na TARURA katika utafiti, usanifu na usimamizi wa rasilimali.

Aidha, kikao hicho kimeazimia kuandaa na kusainiana makubaliano ya mashirikiano baina ya taasisi hizo yatakayolenga katika kubadilishana uzoefu na kufanya tafiti mbalimbali kwa pamoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post