DC TABORA, KIGOMA, WAITAKA EWURA KUONGEZA HAMASA NISHATI SAFI, VITUO VYA MAFUTA VIJIJINI


Wakuu wa Wilaya za Tabora, Mh. Upendo Wella, na Kigoma, Mh. Dkt. Rashid Chuachua, wameipongeza EWURA kwa usimamizi mzuri wa huduma za nishati na maji nchini. Wametoa pongezi hizo walipotembelea banda la EWURA, katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea viwanja vya Ipuli, Tabora, leo, 02.08.2026. 

Viongozi hao wameitaka EWURA kuongeza hamasa kwa wananchi ili kubadili mtazamo na kuhamia katika matumizi ya  nishati safi ya kupikia ili azma ya kufikia 80% ya watumiaji ifikapo 2034 itimie.

Aidha, wameisisitiza EWURA kuendelea kuhamasisha uwekezaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini, wakieleza kuwa  huduma hiyo inahitajika kutokana na kushamiri shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, alitumia fursa hiyo kueleza nafasi ya EWURA ya  kuweka mazingira wezeshi ya kupata wasambazaji wakubwa wa gesi ya mitungi (LPG) katika eneo la Kanda ya Magharibi linalohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma, ambapo kwa sasa ni 19 pekee.

Post a Comment

Previous Post Next Post