MATWEBE AWEZESHA VIFAA VYA UJENZI NYUMBA YA KATIBU UVCCM KIBAHA MJINI


Ndg. Shaban Matwebe "MTOTO WA MKULIMA" Mwenyekiti Mstaafu wa UVCCM Wilaya ya Rufiji akabidhi vifaa vya Ujenzi "UPAUJI" wa Nyumba ya Mtendaji wa UVCCM Kibaha Mjini vyenye Thamani ya Tsh. 3,270,000/= (3.2M) mbele ya Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini.

"Hili ambalo nimelifanya hapa kibaha, tamaa yangu nataka nifanye Mkoa mzima. Kama nitapata ridhaa ya kuombwa michango ya kufacilitate vitu kama hivi vya kuacha alama nipo tayari"

Ameyasema hayo Ndg. Matwebe akiwa anakabidhi Vifaa hivyo akiwasisitiza Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM juu ya umuhimu wa kuacha alama katika majukumu yao ya Uongozi.

Kwa upande wa Umoja wa Vijana wa CCM Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya Ndg. Ramadhan Kazembe amemshukuru Ndg. Matwebe kwa Moyo wake wa Utoaji na kuahidi mashirikiano mazuri baina yao ili Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM iendelee kusonga Mbele.

Post a Comment

Previous Post Next Post