KIKAO KAZI CHA AFISA TARAFA KATERERO, RUWASA NA VIONGOZI WA KATA NA VIJIJI KUJADILI KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI


Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku kwa kushirikiana na Uongozi wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Bukoba chini ya Meneja wake wa Wilaya Eng. Evarist Mgaya na Viongozi wa Kata ya Kemondo na Vijiji vyake viwili Rwagati na Kanazi pamoja na Kijiji cha Katoju, Kata ya Bujugo wamefanya kikao cha pamoja cha kujadili jinsi ya kuendelea kuboresha upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Kikao hiki kimejadili kiundani na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji kwa ubora na kuhakikisha changamoto zote zinafanyiwa kazi.

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kata ya Kemondo imejenga mradi mkubwa wa maji wa Kemondo- Maruku unaogharimu Bilioni 15.8. Mradi huu umeshaanza kutoa huduma kwa wananchi wa Kata 3 za Tarafa ya Katerero ambazo ni Kemondo, Bujugo na baadhi ya maeneo ya Kata ya Katerero huku ukitarajia kunufaisha Kata 7 ukishakamilika wote kwa 100%.

Post a Comment

Previous Post Next Post