Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa akifuatilia kwa umakini mkubwa uwasilishwaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/27 uliowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Khamis Mussa Omar.
Ufuatiliaji huo unaonesha dhamira ya viongozi wa taasisi za umma kufuatilia kwa karibu maelekezo na vipaumbele vya Serikali, hususan katika sekta ya miundombinu ya usafiri na reli ambayo imeendelea kuwa miongoni mwa maeneo ya kimkakati katika kukuza uchumi wa Taifa.
Katika bajeti hiyo, Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa uwekezaji katika miradi mikubwa ya reli ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na abiria pamoja na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha usafiri na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Mkurugenzi Mkuu huyo alifuatilia kwa makini hotuba hiyo akionesha utayari wa TRC kuendelea kute
keleza majukumu yake kwa kuendana na dira na vipaumbele vya Serikali katika kuimarisha sekta ya usafiri wa reli nchini.
