Mapema leo, Mhe. Antony Peter Mavunde, Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Mtumba, ameungana na madiwani wa Jimbo la Mtumba kushiriki hafla fupi ya Umoja wa Makabila ya Dodoma (WAMANGA), iliyofanyika katika Ukumbi wa Ngalya Hall, Dodoma.
Katika hafla hiyo, Mhe. Mavunde na madiwani wake walionesha mshikamano wa hali ya juu kwa kutoa msaada na mchango mbalimbali kwa umoja huo. Miongoni mwa michango hiyo ni fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 5, pamoja na mahitaji mengine muhimu yaliyolenga kuimarisha shughuli za umoja huo.
Hatua hii inaendelea kudhihirisha dhamira ya Mhe. Mavunde ya kushirikiana na wananchi wake, kuimarisha umoja wa kijamii na kusukuma mbele maendeleo ya Jimbo la Mtumba.
Hakika, kazi zinaonekana na matokeo ya uongozi wake yanaendelea kugusa maisha ya wananchi. Hongera Mhe. Antony Peter Mavunde!
