Kongamano la Wanamawasiliano wa Serikali 2026 limeanza rasmi katika Hoteli ya Malaika, jijini Mwanza, likiwakutanisha wataalamu wa mawasiliano ya Serikali kutoka taasisi mbalimbali nchini.
Kongamano hilo linafanyika chini ya kaulimbiu: “Taifa Moja. Sauti Moja. Simulizi za Dira 2050” (One Nation. One Voice. Communicating Vision 2050), likilenga kuimarisha mawasiliano ya Serikali katika kusimulia na kutafsiri utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa wananchi.
Kwa siku kadhaa, washiriki watapata fursa ya kujadili masuala ya kimkakati kuhusu mawasiliano ya Serikali, matumizi ya takwimu na ushahidi katika mawasiliano, kukabiliana na taarifa potofu, pamoja na kuimarisha taswira ya Tanzania katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
Kongamano hili limeandaliwa na Tanzania Association of Government Communication Officers (TAGCO) na linaendelea jijini Mwanza.
