VUNJABEI YAJA NA VUNJABEI BET IMEANZA NA NCHI 7


VUNJABEI GROUP, chini ya Mtendaji Mkuu wake Fred Ngajiro (maarufu kama Fred Vunjabei), leo imezindua rasmi jukwaa jipya la michezo ya kubahatisha (betting) hapa nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na  Biashara Bw. Aristides Robert Mbwasi, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, amempongeza Fred Vunjabei kwa kutafuta fursa nje ya nchi na kuwa mpambanaji, huku akigusia kuwa michezo ya ubashiri imeingizia Taifa Bilioni 260 kwa mwaka 2024/2025.

Jukwaa hili linatarajiwa kufanya kazi si tu ndani ya Tanzania, bali pia katika nchi saba jirani, hatua inayolenga kupanua huduma na kuongeza ushindani katika sekta ya ubashiri wa michezo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Katika utekelezaji wa mradi huo, VUNJABEI GROUP imeingia ubia na kampuni ya kimataifa kutoka nchini Italy, ambayo imewekeza katika teknolojia ya jukwaa hilo. Kwa upande wake, VUNJABEI GROUP imechukua jukumu la kuwekeza katika miundombinu, usimamizi pamoja na masoko katika nchi zote zitakazohudumiwa na mfumo huo.

Sekta ya ubashiri wa michezo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya michezo. Kupitia udhamini wa ligi, vilabu na matukio mbalimbali ya michezo, kampuni za betting zimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza vipaji vya vijana na kuimarisha sekta ya michezo nchini.

Uzinduzi huu unatarajiwa kuongeza ushindani wa kibiashara, kuleta ajira pamoja na fursa mpya za uwekezaji katika tasnia ya michezo na burudani.

Post a Comment

Previous Post Next Post