Kufuatia hatua hiyo ya asilimia 99.7, treni ya mizigo imefanikiwa kufika eneo la Malindi litakalotumika kwa upakuaji na upakiaji wa mizigo bandarini hapo.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipokea jumla ya mabehewa 264 ya mizigo kwaajili ya SGR Desemba 2024.
Kati ya hayo 200 yakiwa ni ya kubebea makontena (containers carriers) na 64 ni ya kubebea mizigo isiyofungwa (loose cargoes).
Kuingia kwa treni ya mizigo eneo la Malindi, ni muendelezo wa TRC wa usafirishaji wa mizigo kati ya Dsm- Dom, toka ilipoanza usafirishaji wa mizigo kwa SGR Juni 27, 2026.
