NCHIMBI AMWAKILISHA RAIS SAMIA MAZISHI YA ASKOFU SHAURI RUVUMA


Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, Marehemu Askofu Stanford Shauri.

Mazishi hayo yamefanyika Liuli, wilayani Nyasa, ambapo Dkt. Nchimbi aliwasilisha salamu za rambirambi za Rais Samia, akieleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa marehemu katika utumishi wa jamii na taifa.

Amesema Askofu Shauri alitoa huduma kwa zaidi ya miaka 12 katika Serikali za Mitaa na zaidi ya miaka 10 kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), akichangia maendeleo ya kijamii na kukuza imani ya Kikristo nchini.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali itaendeleza misingi ya amani na haki ambayo marehemu alisimamia katika utumishi wake.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa, aliishukuru Serikali kwa ushirikiano na taasisi za dini, akitaja pia kuboreshwa kwa barabara ya Mbambabay–Liuli kuwa ni hatua muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post