Waziri wa Maji Tanzania Mhe Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maji na Nishati wa Tajikistan Mhe Juma Daler ambapo amewasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sekta ya Maji kipekee ikiwa ni pamoja na kuipongeza Wizara yake na serikali ya nchi ya Tajikistan kwa ujumla kwa maandalizi mazuri ya Mkutano wa umoja wa Mataifa wa Maswala ya Maji.
Waziri Aweso amekutana na Waziri wa Maji na Nishati Tajikistan mara baada ya kushriki na kuhutubia Mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa wa Maji na Maendeleo Endelevu unaofanyika tarehe 25-28 Mei 2026 jijini Dushanbe nchini Tajikistan.
Katika kikao hicho, viongozi wa Wizara ya Maji Tanzania na Tajikistan wameanzisha mazungumzo ya kushirikiana katika Sekta ya Maji ikiwemo uwekezajikwenye maji na kuimarisha huduma ya maji vijijini na matumizi ya teknolijia sambamba na mikakati ya kujengeana uwezo hususani katika ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi Maji.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso ameeleza mpango unaoendelea kutekelezwa na Sekta ya Maji Tanzania wa Ujenzi wa Gridi ya Taifa ya Maji na kueleza nia ya kuhitaji mashirikiano na Tajikistan katika Utekelezaji huo.
