KAIRUKI AWEZESHA NAULI KWA VIJANA WA KIBAMBA WANAOSOMEA VETA DON BOSCO


Mbunge wa Jimbo la Kibamba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.ANGELLAH JASMIN  MBELWA KAIRUKI ametekeleza ahadi yake ya kuwasapoti vijana wa Jimbo la KIBAMBA ambao walipata fursa ya kuchaguliwa kwenda kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi VETA fursa ambayo ilitolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Kairuki aliwasisitiza vijana hao Wana Kila sababu ya kuendelea kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanafanya vyema katika mafunzo Yao  kwa kuwa vikwazo vidogo vidogo kama nauli havitakuwa sehemu ya kuwakatisha masomo Yao ofisi ya mbunge itaelendelea kutoa sapoti Hadi pale watakapo hitimu Mafunzo hayo kwa kipindi kilichopangwa.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Kairuki aliwashauri vijana hao wanaoendelea na masomo kutengeneza vikundi na kuvisajiri ambavyo vitawawezesha kupata fursa mbali mbali kama za mikopo ambavyo vinaweza  kuwasaidia PINDI pale wanapomaliza mafunzo Yao waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Vile vile, aliwaeleza dhamira yake ya dhati ya kuendelea kuwasaidia na kuwaendeleza Vijana  wa Jimbo la  KIBAMBA katika nyanja Tofauti Tofauti za Kiuchumi, Elimu na Maendeleo kwa Ujumla wake na ninatamani nyinyi mkawe vijana wa Mfano katika Jimbo letu la KIBAMBA. Alisema Mhe KAIRUKI.

Mwisho na kwa umuhimu Mkubwa Mwenyekiti wa Vijana wa wilaya Ndugu SHADRACK MAKANGULA na Katibu wa vijana wa wilaya Ndugu NEHEMIAH PHILEMON walimshukuru mhe. Mbunge kwa namna ambavyo ameendelea kutoa sapoti kwa jumuiya yetu ya Vijana na Vijana kwa Ujumla wake  ndani ya Jimbo la KIBAMBA na hususa kwenye maeneo ya Fursa na uwezeshaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post