MWENGE WA UHURU WAKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA LINGIA-NYAKWALE- KIGAMBONI


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2206, Ndugu Wazo Michael Mwang’onda, leo tarehe 14 Aprili 2026 ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara ya Lingia–Nyakwale yenye urefu wa Km 3.75 mara baada ya kukagua na kuridhika na maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndugu Mwang’onda alipongeza juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na kazi nzuri inayofanywa na mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo.

Aidha, alisisitiza mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi zilizobaki hususan ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua ili kukamilisha mradi kwa wakati na kuondoa adha inayowapata wananchi wakati wa mvua.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Lingia–Nyakwale Km 3.75 unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 8,354,147,684.80 chini ya mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDPII) unaosimamiwa na TARURA.

Utekelezaji wa mradi huo hadi sasa umefikia takribani asilimia 80 na unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji, kupunguza msongamano wa magari pamoja na kuondoa changamoto ya maji ya mvua katika maeneo ya Kibada na Kigamboni kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post