UBUNIFU WA “HAKIKI SCANNER” WAIBUKA KIDEDEA ARUSHA



Kundi la wasichana waliobuni mfumo wa Hakiki Scanner unaohakiki taarifa kwa kutumia Akili Unde (Artificial Intelligence-AI), limeibuka kidedea miongoni mwa makundi sita kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo UDOM, UDSM, Chuo cha Takwimu, IFM, DIT, NIT, ARDHI, IAA (Arusha), Arusha Technical College, SUZA (Zanzibar), India Institute of Technology Madrasa (Zanzibar), MUST pamoja na RUCU baada ya mafunzo ya siku 5. Wanafunzi hawa walifundishwa namna ya kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI) kubuni suluhisho kwa changamoto za jamii.

Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na TCRA, UCSAF na ICTC. Kupitia ushirikiano na wakufunzi kutoka Nelson Mandela, washiriki wanahamasishwa kuvutiwa zaidi na masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM), huku wakijengewa uwezo wa kubuni suluhisho bunifu za kidijitali za kutatua changamoto za kijamii.

Mpango huu ni sehemu ya maandalizi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA (International Girls in ICT Day), inayoadhimishwa kimataifa kila Alhamisi ya mwisho ya mwezi Aprili.

Kaulimbiu ya mwaka 2026:

“Akili Unde kwa Maendeleo: Wasichana Wakibadilisha Mustakabali wa Kidijitali.”

Post a Comment

Previous Post Next Post