Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso akiwa Shangai China amefika katika kiwanda cha KSB Shangai Pump kinachojihusisha na kutengeneza pampu za maji.
Pampu hizi kubwa ni kwa ajili ya maboresho ya mitambo ya Ruvu juu na Ruvu chini kwa kuweka pampu mpya na kuondoa za zamani ambazo ufanisi wake umeshuka na zimekua na matengenezo ya mara kwa mara hivo kusababisha msukumo mdogo na hata kukosekan maji ya uhakika Dar Es Salaam.
Gharama ya pampu hizi ni jumla shilingi bilioni 16.5, ikijumuisha na ufungaji, ambazo zote zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Kazi ya ufungaji inatarajia kukamilika ifikapo Juni 2026.
Mara baada ya mabadiliko ya pamou hizi hali ya huduma ya Maji inatarajiwa kuboreshwa na kuwa ya uhakika zaidi tofauti na sasa.
Lengo Mahususi la timu ya Wizara ya Maji na DAWASA katika ziara hiyo kushuhudia majaribio ya mwisho ya awamu ya pili ya Pampu hizo ambapo Waziri Aweso amejiridhisha na aina, viwango na uwezo wake na kuruhusu mzigo usafirishwe kuleta nchini Tanzania mara moja baada ya matengenezo yake kukamilika.
Aidha, awamu ya kwanza yenye jumla ya Pampu nne ilishakamilika na tayari zimeishafika Dar Es Salaam na kazi ya ufungaji imeanza na inaendelea na baada ya kuwasili kwa hizi kazi itamilishwa na kuwashwa kwa pamoja.
Ununuzi wa pampu hizi ni hatua za makusudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Sululu Hassan kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kupitia Wizara ya maji.
