MBUNGE PONDEZA ATOA SADAKA YA FUTARI KWA WANANCHI CHUMBUNI


Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Ussi Salum Pondeza, ametoa sadaka ya futari kwa wananchi wa jimbo hilo katika hafla iliyofanyika leo Jumapili Februari 28, 2026 katika viwanja vya Salmin Amour visiwani Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sadaka hiyo imelenga kusaidia makundi yenye uhitaji, wakiwemo wazee, yatima na familia zenye hali ngumu za kiuchumi, ili kuwawezesha kupata futari katika kipindi hiki cha ibada.

 Zoezi hilo limeandaliwa, kufadhiliwa na kuratibiwa na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Chumbuni.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mhe. Pondeza amesema

umekuwa utamaduni wake wa kuwashika mkono waislamu wote katika Jimbo hilo ambalo wanatekeleza ibada hiyo kwa kutoa futari ambayo anaamini inasaidia kwa namna moja ama nyingine wahitaji wanaoendelea na mfungo na 

kuwawezesha kutimiza nguzo muhimu ya uislamu wakati huu wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya wanufaika wa sadaka hiyo wameeleza shukrani zao, wakisema kuwa msaada huo umekuja katika kipindi ambacho mahitaji huwa makubwa kwa familia nyingi wakati wa Ramadhani.

Post a Comment

Previous Post Next Post