JENGO ALILOJENGA ALICIA KEYS, TEDROS KUZINDUA FEB.28


Taasisi ya Doris Mollel (@dorismollelfoundation) chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Doris Mollel (@dorismollel), imefanikisha ujenzi wa jengo jipya la kisasa maalum la kwanza nchini kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Watoto njiti) lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Jengo hilo lenye thamani ya Tsh. biljoni 2.125 linatarajiwa kuzinduliwa rasmi February 28,2026 na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Jengo hilo limejengwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Msanii maarufu wa Marekani Alicia Keys inayoitwa KEEP A CHILD ALIVE na ni jengo maalum kwakuwa linaenda kuhamasisha zero separation (Mtoto kutotengwa na Mama yake), na lina chumba maalum kwa ajili ya Baba kumuona Mama na Mtoto wake akiwa Hospitalini hapo na lina uwezo wa kuhudumia Watoto 42 kwa wakati mmoja.

Doris Mollel amesema baada ya kukamilisha ujenzi Kwimba, Taasisi hiyo itakwenda pia kujenga majengo kama hayo kwenye Mikoa mingine ikiwemo Dar es salaam, Wilaya tatu za Mwanza, Wilaya mbili za Shinyanga na Geita, Tabora pamoja na Zanzibar ambapo lengo ni kujenga Hospitali nyingine 10 hadi kufikia mwaka 2028.

Post a Comment

Previous Post Next Post