MBUNGE WA VUNJO AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYANZO VYA MAJI, ATOA MAELEKEZO MAHUSUSI


Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Mhe. Enock Koola, ametembelea vyanzo vitatu vya maji vilivyopo katika kata tatu tofauti jimboni humo hii wiki kwa lengo la kukagua changamoto za upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Vyanzo vilivyotembelewa ni Chanzo cha Kizumbe kilichopo Kijiji cha Mshiri, Kata ya Marangu Mashariki; Chanzo cha Kiwindo kilichopo Kijiji cha Komakundi, Kata ya Mamba Kaskazini ambacho kwa sasa kimekauka kutokana na kiangazi; na Chemchem ya Nsirwe kilichopo Kijiji cha Kimangara, Kata ya Mamba Kusini.

Ziara hiyo imehusisha viongozi wa kata na vijiji, ikiwemo Diwani wa Kata ya Mamba Kusini,  Reward Minja, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, pamoja na wazee mashuhuri waliokuwa wadau wa maendeleo. 

Viongozi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWASA) pia walishiriki kikamilifu katika ziara hiyo.

Kupitia ziara hiyo, Mhe. Mbunge amebaini changamoto kadhaa ikiwemo uzembe wa baadhi ya mafundi wa MUWASA, ambao hawakusimamia majukumu yao kwa weledi unaotakiwa. 

Kufuatia hilo, baadhi ya changamoto zilianza kutatuliwa mara moja, huku hatua za kisera na kisheria zikisalia kufanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine, Mbunge Koola ameelekeza uongozi wa MUWASA kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ili kutatua changamoto zilizopo na ameahidi kuzipitisha hoja muhimu bungeni ili Serikali ichukue hatua za kudumu kwa manufaa ya wananchi wa Jimbo la Vunjo.

Post a Comment

Previous Post Next Post