DKT.ABBASI TUZO ZA SERENGETI KURA 132,874 ZAPIGWA NI USIKU WA KUACHA ALAMA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amesema kwa maandalizi aliyoelezwa katika kikao na Kamati ya Maandalizi, anaamini Tuzo za Utalii na Uhifadhi (Serengeti Awards) 2026 zinakwenda kuacha alama kwa wadau wa sekta hizo.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Januari 25, 2026, jijini Dar es Salaam katika kikao cha maandalizi ya Tuzo hizo kilichohudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kuelekea Usiku wa Tuzo Januari 31, 2026 jijini Arusha. 

“Nawapongeza kwa maandalizi mazuri na naamini tuzo hizi pamoja na kwamba kila mtu hawezi kuwa mshindi lakini zitaacha alama chanya kwa wale ambao mwaka huu watashinda ili kuchagiza wengine kujipanga zaidi mwakani,” alisema Dkt. Abbasi.

Alisema ili kuhakikisha Tuzo hizo zinakuwa na ubora na kuaminika jopo huru nje ya Kamati ya Maandalizi lenye majaji wabobezi katika sekta za utalii, malikali, misitu na wanyamapori limeindwa na linajifungia kufanya mchujo na kuangalia kura za wadau. 

Ameeleza kuridhishwa na wadau wanaoendelea kujitokeza kupiga kura kupitia tovuti ya www.serengetiawards.go.tz ambapo mpak leo zaidi ya kura 132,874 zimepigwa. Mwisho wa kupiga kura ni Januari 27, 2026.

Post a Comment

Previous Post Next Post