Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba aliyechaguliwa hivi karibuni ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mikoni iliyopo ndani ya Tarafa ya Katerero Mhe. Sadoth Ijunga leo Alhamisi Disemba 18, 2025 amemtembelea Ofisini kwake Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku na kufanya mazungumzo ya kimkakati kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya Tarafa ya Katerero na Halmashauri nzima ya Bukoba ambayo Mhe. Ijunga anaiongoza.
Afisa Tarafa Katerero amemuahidi ushirikiano wa 100% huku akimpongeza kwa imani ya wananchi wa Mikoni kumchagua kuwa Diwani kwa kipindi cha pili huku madiwani wenzake wote wa Halmashauri ya Bukoba wakimchangua kwa kura zote kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri akipokea kijiti kutoka kwa Mtangulizi wake Mhe. Murshid Ngeze.
Kikao hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri kilihudhuriwa pia na Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cyriacus Sosthenes, Afisa Tarafa ya Kyamtwara Bi. Dorika Rubete na Kaimu Afisa Tarafa Bugabo Ndugu Bruno Kahwa.
