MKURUGENZI MKUU WA TCRA AKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI MTANDAONI;


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari amefanya kikao kazi na watoa huduma ya utangazaji kwa njia ya mtandao, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yatakayoendelea kukuza sekta ya utangazaji na kuchochea matumizi chanya ya mitandao kwa vijana ili kujiongezea kipato.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Dkt. Bakari amesema TCRA inatambua mchango wa watoa huduma za maudhui mtandaoni katika kuongeza maudhui ya ndani yenye tija (local content), hivyo ni muhimu kuwa na majadiliano ya namna bora ya kuendelea kuunga mkono jitihada za vijana wanaotumia mitandao kama sehemu ya ajira.

Baadhi ya watoa huduma za maudhui mtandaoni wameiomba TCRA kuboresha Kanuni za Utangazaji ili kuendana na mazingira yaliyopo sasa pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watoa huduma hao ili kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi.

Kikao kazi hicho ni mwendelezo wa jitihada za TCRA kukutana na wadau wake ili kuboresha sekta ya mawasiliano inayochangia ukuaji wa uchumi wa kidijiti.


Post a Comment

Previous Post Next Post