MATAGI MIONGONI WA MAWAKILI 774 WALIOAPISHWA JIJINI DODOMA KUWA WAKILI


Jumla ya mawakili wapya 774 wameapishwa leo katika Mahafali ya 73 ya Uwakili yaliyofanyika jijini Dodoma, tukio lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, mahakama, na vyombo vya ulinzi na usalama.

Miongoni mwa waliopishwa ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Georgina Matagi, ambaye ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD).

SSP Matagi ameweka historia kwa kuwa mmoja wa maafisa wa Polisi waliomaliza mafunzo ya sheria na kuapishwa kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa hatua hiyo, SSP Matagi sasa anakuwa miongoni mwa maafisa wa Polisi waliobobea katika taaluma ya sheria, hatua inayomwezesha kuendesha kesi mahakamani kama wakili mwenye sifa kamili.

Tukio hili linaakisi ukuaji wa taaluma ya sheria nchini na kuimarika kwa ushirikiano baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na mhimili wa mahakama katika kulinda haki na utawala wa sheria.

Katika hotuba yake, mmoja wa viongozi wa Mahakama alisisitiza umuhimu wa mawakili kuzingatia maadili ya taaluma,uadilifu na kutetea haki za wananchi kwa ujasiri na uaminifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post