𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜


"𝘙𝘢𝘪𝘴 𝘔𝘩𝘦. 𝘋𝘬𝘵. 𝘚𝘢𝘮𝘪𝘢 𝘚𝘶𝘭𝘶𝘩𝘶 𝘏𝘢𝘴𝘴𝘢𝘯 𝘢𝘮𝘦𝘶𝘯𝘥𝘢 𝘛𝘶𝘮𝘦 𝘺𝘢 𝘬𝘶𝘤𝘩𝘶𝘯𝘨𝘶𝘻𝘢 𝘺𝘢𝘭𝘪𝘺𝘰𝘵𝘰𝘬𝘦𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘷𝘶𝘳𝘶𝘨𝘶 𝘻𝘢 𝘖𝘬𝘵𝘰𝘣𝘢 29, 𝘵𝘶𝘮𝘦 𝘣𝘢𝘥𝘰 𝘩𝘢𝘪𝘫𝘢𝘭𝘦𝘵𝘢 𝘳𝘪𝘱𝘰𝘵𝘪 𝘭𝘢𝘬𝘪𝘯𝘪 𝘵𝘢𝘺𝘢𝘳𝘪 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘰𝘬𝘦𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘪𝘱𝘪𝘯𝘨𝘢 𝘵𝘶𝘮𝘦 , 𝘫𝘪𝘶𝘭𝘪𝘻𝘦𝘯𝘪 𝘬𝘸𝘢𝘯𝘪𝘯𝘪 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘰𝘨𝘰𝘱𝘢 𝘵𝘶𝘮𝘦 𝘪𝘴𝘪𝘧𝘢𝘯𝘺𝘦 𝘬𝘢𝘻𝘪 𝘺𝘢𝘬𝘦 ? 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘶𝘮𝘪𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘢 𝘮𝘢𝘵𝘢𝘪𝘧𝘢 𝘺𝘢 𝘯𝘫𝘦 𝘯𝘥𝘪𝘰 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘢𝘬𝘢 𝘵𝘶𝘮𝘦 𝘪𝘵𝘰𝘬𝘦 𝘯𝘫𝘦...𝘵𝘶𝘴𝘶𝘣𝘪𝘳𝘪 𝘵𝘶𝘮𝘦 𝘪𝘭𝘦𝘵𝘦 𝘳𝘪𝘱𝘰𝘵𝘪 𝘯𝘢 𝘴𝘦𝘳𝘪𝘬𝘢𝘭𝘪 𝘪𝘵𝘢𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘬𝘢𝘻𝘪 𝘺𝘢𝘬𝘦"

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. 𝗞𝗲𝗻𝗮𝗻𝗶 𝗞𝗶𝗵𝗼𝗻𝗴𝗼𝘀𝗶 wakati wa mkutano wake na Viongozi wa Chama na Jumuiya wa mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo tarehw 06 Disemba 2025.

Mwenezi Kenani amebainisha kuwa kumekuwa na baadhi ya watu ambao ni walanguzi na wasiopenda kuona Tanzania ina amani ambao ndiyo wanatumika katika kuchochea vurugu nchini ambao watu hao baadhi hawapo nchini na wengine hata urai wa Tanzania walishaukataa na wanatumiwa kwa kazi za kushinda mitandaoni kutukana serikali, Chama Cha Mapinduzi, Viongozi pamoja na kuhamasisha machafuko ya amani.

"𝘛𝘶𝘭𝘪𝘯𝘥𝘦 𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘺𝘦𝘵𝘶, 𝘵𝘶𝘴𝘪𝘸𝘦 𝘸𝘢𝘫𝘪𝘯𝘨𝘢 𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘩𝘢𝘳𝘪𝘣𝘶 𝘯𝘺𝘶𝘮𝘣𝘢𝘯𝘪 𝘵𝘶𝘭𝘪𝘱𝘰𝘻𝘢𝘭𝘪𝘸𝘢, 𝘩𝘢𝘱𝘢 𝘯𝘥𝘪𝘰𝘰 𝘵𝘶𝘵𝘢𝘬𝘢𝘱𝘰𝘻𝘪𝘬𝘪𝘸𝘢.."

"..𝘩𝘢𝘰 𝘸𝘦𝘯𝘨𝘪𝘯𝘦 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘩𝘢𝘮𝘢𝘴𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘷𝘶𝘳𝘶𝘨𝘶 𝘬𝘸𝘢𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘸𝘢𝘱𝘰 𝘯𝘫𝘦 𝘺𝘢 𝘛𝘢𝘣𝘻𝘢𝘯𝘶𝘢 𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘸𝘢𝘱𝘦𝘯𝘥𝘪 𝘛𝘢𝘪𝘧𝘢 𝘭𝘦𝘰 𝘯𝘥𝘪𝘺𝘰 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘦𝘯𝘨𝘪𝘯𝘦 𝘩𝘢𝘵𝘢 𝘶𝘳𝘢𝘪𝘢 𝘸𝘢 𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘩𝘪𝘪 𝘸𝘢𝘮𝘦𝘶𝘬𝘢𝘵𝘢𝘢...𝘮𝘵𝘶 𝘩𝘶𝘺𝘰 𝘢𝘯𝘢𝘱𝘢𝘵𝘢 𝘸𝘢𝘱𝘪 𝘶𝘻𝘢𝘭𝘦𝘯𝘥𝘰 𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘪𝘱𝘦𝘯𝘥𝘢 𝘛𝘢𝘯𝘻𝘢𝘯𝘪𝘢 𝘬𝘢𝘮𝘢 𝘩𝘢𝘵𝘢 𝘶𝘳𝘢𝘪 𝘩𝘢𝘯𝘢? "

"𝘩𝘢𝘵𝘶𝘯𝘢 𝘴𝘢𝘣𝘢𝘣𝘶 𝘺𝘢 𝘬𝘶𝘰𝘨𝘰𝘱𝘢 𝘸𝘢𝘭𝘢 𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘵𝘢𝘩𝘢𝘳𝘶𝘬𝘪, 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘶𝘮𝘪𝘢 𝘬𝘪𝘭𝘢 𝘮𝘣𝘪𝘯𝘶 𝘬𝘶𝘵𝘢𝘧𝘶𝘵𝘢 𝘥𝘰𝘭𝘢, 𝘸𝘢𝘮𝘦𝘴𝘩𝘪𝘯𝘥𝘸𝘢 𝘬𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦 𝘴𝘢𝘯𝘥𝘶𝘬𝘶 𝘭𝘢 𝘬𝘶𝘳𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘢𝘬𝘢 𝘬𝘶𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘶𝘤𝘩𝘰𝘤𝘩𝘦𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘷𝘶𝘳𝘶𝘨𝘢 𝘢𝘮𝘢𝘯𝘪 𝘺𝘦𝘵𝘶, 𝘵𝘶𝘴𝘪𝘬𝘶𝘣𝘢𝘬𝘪 𝘵𝘶𝘪𝘭𝘪𝘯𝘥𝘦 𝘢𝘮𝘢𝘯𝘪 𝘺𝘢 𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘺𝘦𝘵𝘶"

Aidha, Mwenezi Kenani ameeleza kuwa yapo baadhi ya Mataifa yasiyopenda kuona Watanzania wanishi kwa amani, hawabaguani kwa dini wala ukabila, mataifa hayo ndiyo yanaongoza ajenda za uchochezi wa kuvuruga amani yetu ambayo mengine ni kutokana na kukosa walichokuwa wakikitaka nsani ya Taifa letu wakiita ni maslahi yao huku akissitiza kuwa hakuna mwenye maslahi ndani ya Tanzania zaidi ya Watanzania wenyewe.

Post a Comment

Previous Post Next Post