Wataalamu kutoka Benki ya Dunia wakishirikiana na wataalamu kutoka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wamekagua maendeleo ya barabara zinazojengwa mkoani Iringa katika wilaya ya Iringa, Mufindi na Kilolo.
Barabara hizo ni Mtili-Ifwagi iliyopo Mufindi na Wenda-Mgama iliyopo wilaya ya Iringa zinazojengwa na TARURA huku upande wa TANROADS ni barabara ya Iringa-Kilolo.
Ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa kwa kiwango cha lami kutakuwa na taa za barabarani, vivuko vya waenda kwa miguu pia njia za watembea kwa miguu.
Kwa upande wa uondoaji wa vikwazo barabarani (bottlenenck) wataalamu wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madaraja yaliyopo Mufindi na Kilolo.
Mradi wa RISE ni mradi unaotekelezwa na TARURA na TANROADS kwa mkopo nafuu wa dola milioni 350 kutoka Benki ya Dunia.