KIJIJI KWA KIJIJI, NYUMBA HADI NYUMBA KATA YA KISEGESE - MKURANGA


Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga ndugu @abdallahulega  na team nzima ya Chama cha mapinduzi Wilaya ya Mkuranga Wameendelea na Kampeni yao ya kisayansi kwa kupita nyumba kwa nyumba pia mtu kwa mtu kutafuta kura za kishindo za Wagombea wa Chama cha Mapinduzi.

Ndugu Ulega amekuwa akimuombea Kura nyingi za ndio Kwa Mgombea wa kiti cha  Urais kupitia Ccm ndugu Dkt @samiasuluhuhasani kwa kila kundi la wananchi, ikiwemo Wakina Mama, Wazee, boda boda, Vijana, Wakulima na Wafugaji katika Kata ya Kisegese wilayani Mkuranga.

Aidha, Mgombea wa Ubunge jimbo la mkuranga ametoa ahadi kadhaa kwa wananchi wengi waliojitokeza kwenye Mkutano mkubwa wa adhara uliofanyika viwanja vya kijiji cha Chamgoi ikiwemo 

1. Uboreshwaji wa mtandao wa Barabara ili kunganisha vijiji na vitongoji vyote vya kata ya kisegese.

2. Kujenga na kuboresha vituo na  huduma za Afya ikiwemo kuongeza vifaa tiba.

3. Kujenga na kuboresha miundombinu ya Maji, Umeme na Elimu ili kuifungua zaidi kata ya kisegese kwenye Maendeleo.


Hitimisho, Wananchi wa kata ya Kisegese  Wamewahakikishia Uongozi wa Ccm Wilaya ya Mkuranga  na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo la Mkuranga ndugu @abdallahulega  Kura nyingi za kishindo na za Heshima kwa Rais DKT @Samiasuluhuhasani ifikapo October 29 asuhuhi na mapema.

Post a Comment

Previous Post Next Post