Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa wito kwa wananchi nchini kujitokeza katika Ofisi za TRA nchini ili kupata Huduma mbalimbali Jumamosi ya leo Tarehe 21, Juni,2025 ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuboresha Huduma zake kwa wananchi ambao hawapati muda wa kufika ofisini siku za kazi.
TRA imesema kuwa hiyo ni nafasi maalumu kwa wananchi ambao hawapati muda wa kufika ofisini siku za kazi hivyo kuwa Jumamosi hii itamuwezesha mwananchi kufika ofisi yoyote ya TRA nchini na kupata Huduma bila usumbufu ambapo Huduma zitatolewa kuanzia saa mbili na nusu asubhi hadi saa kumi na moja jioni.
Miongoni mwa Huduma zitakazotolewa ni usajili wa TIN, ukadiriaji, kutoa control namba, kulipa madeni,kusaidia usajili na kuhamisha umiliki wa vyombo vya moto, kupokea na kutatua changamoto za walipakodi na kwa maelezo zaidi mteja wasiliana kupitia namba za 0800780078 au 0800750075 au tuma ujumbe mfupi kwa barua pepe: huduma@tra.go.tz Tovuti: www.tra.go.tz.
Aidha TRA imesisitiza kuwaJumamosi hii ya Juni, 21, 2025 ni nafasi ya pekee walipakodi kuja kukadiriwa na kulipa madeni yao kwa kuwa ni mwisho kabisa wa kulipa kodi awamu pili na mwisho wa kuleta ritani pamoja na kulipa kodi ya mapato kwa makampuni.
Kodi yetu .Maendeleo yetu “Pamoja tunajenga Taifa Letu"