SHEIKHE PONDA: WAISLAMU WOTE TUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU


Waislamu wote nchini Tanzania, wameaswa kujiandaa na kushiriki Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, wabunge na madiwani, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Shura ya Maimamu katika salamu za Sikukuu ya Eid, ukisema kuwa wananchi kushiriki katika uchaguzi huo ni sehemu sahihi ya kuchagua viongozi wenye sifa na uadilifu kwa maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Taarifa iliyotumwa leo Juni 7, 2025 katika vyombo vya habari na kutiwa saini na Katibu Mkuu Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikhe Ponda Issa Ponda ilisema wanawakumbusha Watanzania umuhimu wa kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa ngazi mbalimbali kwa kuwa ndio kanuni ya uboreshaji wa maisha na kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla. 

“Tunatoa wito kwa Waislamu wote kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani Oktoba 2025, na kuchagua viongozi wenye sifa ya uadilifu, ujuzi na wenye historia ya kutumikia na kupigania maslahi ya Umma. Tunawakumbusha umuhimu wa kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa ngazi mbalimbali kwa kuwa ndio kanuni ya uboreshaji wa maisha na kuleta maendeleo ya Taifa kwa ijumla,” ilisema taarifa hiyo ya Shura ya Maimamu inayoongozwa na Sheikhe Ponda.

Vyama mbalimbali vimeendelea kufanya maandalizi ya kushiriki Uchaguzi huo ukiacha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wamekosa sifa ya kushiriki uchaguzi huo kutokana na kushindwa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi huo zilizoandaliwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post