TARURA YAENDELEA KUWEKA WAZI VIWANGO VYA FIDIA KWA MRADI WA BARABARA MASUMBWE–IPONYA


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) imefungua zoezi la kuweka wazi viwango vya fidia kwa waathiriwa wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Masumbwe-Iponya- Nyashimba yenye urefu wa Km 20 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Zoezi linaratibiwa na kusimamiwa na wataalamu wa TARURA wakishirikiana na Wataalamu Washauri wa Tathmini za Kimazingira na Kijamii, Mpango wa Uhamishaji Watu na Makazi na Usanifu chini ya mradi wa RISE unaogharamiwa na mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.

Barabara hiyo inayounganisha vijiji vya Masumbwe, Shenda, Iponya, Buluhe na Nyashimba katika kata za Masumbwe na Iponya inatarajiwa kuboresha shughuli za kijamii na  kiuchumi ikiwemo kilimo, ufugaji na uchimbaji madini.

Post a Comment

Previous Post Next Post