WASANII WASHEREHEKEA KUZALIWA KWA RAIS SAMIA KWA KUHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI SAFI



Wasanii mbalimbali Wakiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wamejumuika pamoja na wapishi/wakaanga samaki katika soko la Samaki Feri jijini Dar es Salaam leo Januari 27, 2025, katika kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na hilo, wasanii hao wakiongozwa na Lamata Leah kutoka Lamata Village wamegawa mitungi ya gesi kwa wapishi wa Samaki katika eneo hilo kama hatua muhimu katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuhamisha Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.

Kwa upande wa wapishi wa Samaki, wameshukuru wasanii hao kwa kuwatembelea na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rais Samia pamoja nao, huku wakitumia fursa hiyo kutuma salamu za pongezi kwa Rais Samia kwa kuchaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi utakaofanyika baadae mwaka huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post