WIZARA YA MADINI, FARU GRAPHITE WAJADILI CHANGAMOTO ZA MAENDELEO YA MRADI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Oktoba 07, 2024 aliongoza kikao kati ya Wizara na Kampuni ya Faru Graphite Corporation kilicholenga kujadili maendeleo ya Mradi wa uchimbaji Madini ya Kinywe  wa Faru Graphite unaotekelezwa katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, Mbibo aliihakikishia kampuni hiyo kushughulikia changamoto inazokabiliana ikiwemo kifungu 56 na 10 cha Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Madini na sheria zingine  ili kuuwezesha  mradi huo kutekelezwa kwa wakati.

 Faru Graphite Corporation ni kampuni ya ubia kati yake na Serikali ya Tanzania ambapo Serikali ina umiliki wa hisa zisizofifishwa za asilimia 16 na kampuni ya Black Rock Limited yenye hisa asilimia 84

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Faru Graphite Corporation Bw. John de Vries na Mkurugenzi wa Black Rock Mining masula ya fedha  Bw. Paul Sims  alieleza kwamba kampuni hiyo imeweza kushughulia masuala kadhaa ikiwemo changamoto ya umeme na  upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa mradi ili kuhakikisha unatekelezwa kwa wakati.

Pia, de Vries alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Madini kwa ushirikiano inaoutoa katika kutatua changamoto zinazoikabili, na kuongeza kwamba, Wizara iendelee na ushirkiano huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post