MBUNGE MAHAWANGA AZINDUA GULIO LA WAJASIRIAMALI WANAWAKE MBWENI


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth ameungana na Umoja wa Wajasiriamali Wadogo Wanawake wa Kata ya Mbweni (Mbweni Women Enterpreneurs) katika uzinduzi wa gulio ambalo linawaunganisha Wajasiriamali wote ndani ya Kata ya Mbweni.

Mh. Mahawanga amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono juhudu za Wanawake wajasiriamali nchini na kuhakikisha anaendelea kutafuta fursa mbalimbali zinazoendelea kustawisha uchumi wa Wanawake katika shughuli zao mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Mh. Mahawanga ameendelea kuwahamasisha Wanawake wajasiriamali wote ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kufanya kazi kama timu kama ilivyo Kata ya Mbweni ili kupata matokeo ya haraka na kutunza mitaji yao isipotee, kwani ni lazima kuwa na malengo katika shughuli zao za ujasiriamali na kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali, Taasisi za kifedha na Mashirika yanayounga mkono juhudi za kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Mh. Mahawanga amempongeza sana Mbunge Mstaafu wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, mama Zarina Madabida kwa kuendelea kuwashika mkono wanawake wajasiriamali hasa kuwa mlezi wa wanawake hao ndani ya Kata ya Mbweni na kumuahidi kuwa atakuwa naye bega kwa bega kuhakikisha wanatimiza malengo yao ili kuleta chachu kwa Kata zingine kwani ni sehemu ya mikakati yake kuhakikisha Wajasiriamali wote wanaungana na kushikana mikono bila kuwaacha wengine nyuma.

Aidha Mhe. Mahawanga amewasihi sana Wanawake Wajasiriamali ndani ya Mkoa wa Dar ea Salaam kutumia muungano wao kuhakikisha wanajiandikisha na wanashiriki kikamilifu kwenye zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mtaa, vile vile wenye sifa muda utakapofika wakachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo kwani yeye anaamini Wanawake ni viongozi wazuri na waaminifu sana.

Mwisho Mh. Mahawanga ametoa wito kwa Wanawake wote Wajasiriamali kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo ndani ya Kata zao na Mkoa wa Dar es Salaam kwani yeye yupo pamoja nao katika kila hali na lengo lake kubwa ni kuhakikisha Wajasiriamali wote wanaungana katika vikundi, kutafuta masoko, fursa elimu ya utunzaji fedha ili hata tunapotafuta wadau watukute kwa wingi na umoja wetu ndani ya Kata zetu badala ya kuwa mmoja mmoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post