Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ametembelea na kukagua Mradi wa Miji 28 Chato mkoani Geita.
Mradi huu una Thamani Bil 38 na unatekelezwa na Mkandarasi Afcon wa India.
Katika ziara hii Waziri Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri.
Aidha Waziri Aweso ameelekeza kazi ya utekelezaji wa Mradi huu ifanyike usiku na mchana na kwa kasi kwani ni Mradi tegemeo kwa wananchi wa Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla zaidi akisisitiza usimamizi na ufuatilaji toka kwa watendaji wa Wizara ya Maji waliopewa wajibu huo.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewahakikishia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwamba wataalamu wa Wizara ya Maji wataifanya kazi ya utekelezaji wa Mradi huu kwa weledi, wakati na thamani ya fedha.