AWESO AWEKA MKAKATI UTEKELEZAJI WA MPANGO MAJI ASILIMIA 95 MIJINI NA 85 VIJIJNI


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo tarehe 12 August 2024 Wizara ya Maji Mtumba Dodoma amefanya kikao kazi cha Kimkakati na Watendaji wa Sekta ya Maji akiwa na lengo mahususi la kuweka mikakati ya utekelezaji wa Mpango Ilani ya Uchaguzi kuhakikisha kufikia 2025 Upatikanaji wa Maji mijini unafikia 95% na Vijijini 85%.

Aidha Aweso ametoa maelekezo mbalimbali, miongozo, mikakati na mipango ya namna gani lengo hili ambalo pia ni kipaumbele chaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika dhamira yake ya kumtua Mama ndoo Kichwani.

Hali ya upatikanaji wa Maji kwasasa ni mijini ni asilimia 90% na vijijini asilimia 79.6

Waziri Aweso ameyasema hayo alipokutana na uwakilishi makundi yote muhimu ya Wizara ikiwa ni pamoja na baadhi ya wenyeviti wa Bodi, Menejiment ya Wizara na RUWASA, Wawakilishi wa wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Maji na Mameneja wa Mikoa na Wilaya Maji Vjijini (RUWASA) sambamba na Wawakilishi wa Idara na vitengo vyote vya Wizara.

Pia Mhe Aweso amewaalika wazee wataalamu wastaafu wa Wizara hiyo katika kuhakikisha wanatoa mawazo yao katika utekelezaji wa Mpango huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post