ZINGATIENI LISHE BORA KWA WANAFUNZI- KATIMBA


WAKUU wa shule za sekondari za bweni wametakiwa kuzingatia suala la lishe kwa wanafunzi ili kuwakuza kimwili na kiakili.

Mhe.Katimba ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya elimu hususani kwa shule za wasichana za sayansi ya mkoa wa Geita.

“Tusisahau pia kwenye upande wa lishe kwasababu unapotaka mtoto awe na uwezo wa kupokea na kupata elimu bora basi tuna kila sababu ya kijana huyu kupata lishe iliyobora.”amesisitiza Katimba

Amesema katika kutimiza hilo ni vyema kutumia mazingira yaliyopo kupanda miti ya matunza na kuwafundisha wanafunzi  stadi za kazi ikiwemo  kulima mbogamboga.

Pia amewataka kuhakikisha nafaka zinazotumiwa na wanafunzi kama chakula hususani mahindi hayakobolewi ili wapate lishe za nafaka hizo.

“Tunaweza kusaidia kufikia dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu yameletwa majengo mazuri kama haya ili mtoto apate elimu bora, wanaltewa walimu wa sayansi, lakini lishe ni sehemu muhimu sana ya wao katika mazingira ya shule kukua kimwili na kiakili ili kuweza kupokea elimu nzuri wanayopatikwa.” amesema Katimba

“Napenda kuwakumbusha wajibu wa msingi kwa uongozi wa shule mzingatie kutengeneza mazingira ya kuwa na bustani, kupanda miti ya matunda na pia kutokukoboa nafaka ambazo tunawalisha wanafunzi wetu .

Sambamba na hilo, pia  Mhe.Katimba  amezitaka mamlaka za Serikali za mitaa kuwa wabunifu kwa kubuni  miradi na vyanzo vya uhakika vya mapato.

Post a Comment

Previous Post Next Post