Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Charles Mahera amesema Serikali imetoa kibali cha ajira kwa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora kwaajili ya kuajiri Maafisa Ustawi wa Jamii 350 katika Halmashauri zote ambazo zina uhaba wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika mwaka huu wa fedha 2024/25.
Hayo yamesemwa kwaniaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Bi. Subisya Kabuje katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora wakati akiongea na timu ya usimamizi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wakati wa tathimini ya Ziara ya siku mbili iliyofanyika Mkioni hapo kwaajili ya kufatilia huduma mbalimbali za Ustawi wa Jamii zinatekelezwa katika Mkoa huo.
Amesema kutokana na ongezeka la vitendo vya ukatili katika jamii, wananchi wamekuwa wakiende katika sehemu zisiso sahihi pindi wanapokubwa na changamoto hizo kutokana na uhaba huo wa Watumishi katika baadhi ya maeneo, hivyo Serikali imeona ni vyema kuongeza wataalamu wa maswala ya kijamii ili kuweza kusaidia jamii kuwa na ustawi bora.
Pia amesisitiza kuwa kutokana na taarifa mbalimbali zinazoendelea za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto maafisa Ustawi wa Jamii kuwa na tabia ya kufatilia Watoto wanaoishi katika mazingira hatari katika Halmashauri zao na kutoa elimu watu wanao wazunguka.
“Kama mnavyojua saizi kumekuwepo na wimbi la vitendo vya ukatili kwa Watoto kwahiyo Maafisa Ustawi wa Halmashauri wanapaswa kujipanga kutoa elimu kuhusu maswala ya ukatili na madhara yake kwa ngazi ya kata na vijiji”
Aidha Bi. Kabuje amemuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuendelea kusimamia utegwaji wa Fedha kwaajili ya ununuzi wa Mafuta maalumu kwaajili ya watu wenye ulemavu wa Ngozi katika Malmashauri za Mkao wa Tabora.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Margaret Simwanza Sitta ameipongeza na kushukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa namna inavyosimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu na Afya katika Halmashauri ya Urambo.