SEKTA YA MAJI HAINA DENI NA MH.RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (Mb) ameweka bayana kuwa Wizara ya Maji haina deni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa wa miradi ya Majisafi Nchini hususani Mkoa wa Dar es salaam.

Mhe Aweso ameyasema hayo wakati akitoa mrejesho wa ziara yake ya siku tano mkoani Dar es salaam kukagua uhakika wa upatikanaji wa maji na kupunguza changamoto za kihuduma

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan haina deni sekta ya Maji, ni jukumu letu sisi kuhakikisha uwekezaji huu unaleta tija kwa Wananchi na sisi ndio watekelezaji wa vitendo vya uwekezaji huu” alisema Mhe Aweso.

Katika mahojiano hayo, Mhe Aweo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri

Post a Comment

Previous Post Next Post