WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA TOA 2024.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa mapema leo Juni 12, 2024 amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA ili kushiriki kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Taasisi ya maboresho ya Serikali za mitaa Tanzania (TOA).

Mkutano huo unafanyika Kwenye Kituo cha kimataifa cha Mikutano Arusha AICC ukiwahusisha Makatibu tawala wa Mikoa yote ya Tanzania bara, Wakurugenzi watendaji wa Majiji, Miji na Halmashauri zote 184 pamoja na Maofisa wote wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote pamoja na Wakurugenzi wa Manispaa zote na wasimamizi wa Mamlaka za serikali za Mitaa kwa upande wa Zanzibar.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu pamoja na Missaile Albano Musa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kando ya Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi na serikali.

Kufanyika kwa mkutano huu wa siku tatu wa TOA ni muendelezo wa fursa nyingine muhimu kwa Wakazi wa Arusha ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekuwa akisisitiza mara zote umuhimu wa wakazi wa Arusha kutumia kikamilifu fursa za kiuchumi na za kijamii za uwepo wa wageni mbalimbali wanaofika Mkoani hapa kwaajili ya mikutano na warsha za kitaifa na Kimataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post