VIONGOZI WA DINI WATAKA TWITTER IFUNGWE TANZANIA


Viongozi wa dini waiomba serikali kuufungia mtandao wa kijamii wa Twitter ( X ) nchini kwani mtandao huo umeonekana ukivunja maadili na taratibu za nchi kwa kuhamasisha ushoga na usagaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 11,2024 Mwenyekiti mstaafu wa Baraza Kuu la Waislam Vijana Tanzania na Mhadhiri mkubwa  Shekh Alhaji Sulle amesema kufuatia na Dunia kuingia katika utandawazi kumepelekea kumomonyoka kwa maadili na kupelekea kuharibu taswira ya nchi.

Amesema mtandao wa Twitter (X) umekuwa ukihamasisha mapenzi ya jinsia moja na ushoga jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

"Tunawajibu wa kuyapima mambo ambayo tunaletewa ambayo yapo kinyume na maadili tunapaswa kuyapinga vikali ili kulinda maadali na tamaduni zetu za Kitanzania na kulinda kizazi kilichopo sasa na kijacho," amesema.

Kwa upande wake, Askofu Allen Siso amesema madhara yanayotokana na kuruhusu mtandao huo kwa jamii ni kukosa kizazi chenye maadili na kuvunja tamaduni za nchi ambapo ameiomba Serikali kupitia Bunge na Wizara husika ichukue hatua za haraka kuufungia mtandao huo ili kulinda tamaduni na maadili ya nchi lakini pia kufuata maandika ya neno la Mungu ambayo yanapinga vikali vitendo hivyo vya usagaji na mapenzi ya jinsia moja.

Post a Comment

Previous Post Next Post